Mjasiriamali Mbunifu

 

 

Kuwezesha Ubunifu katika Kilimo, Ufugaji & Biashara

AJE-FARMS tunaamini kwamba ubunifu na uvumbuzi ni muhimu ili kuleta mabadiliko katika sekta ya kilimo. Mradi huu unasaidia wakulima, wajasiriamali na wavumbuzi wa mifumo au mbinu za kilimo na ufugaji kuweza kubadili ubunifu wao kuwa biashara kubwa inayoweza kukuza uchumi wao na jamii kwa ujumla. Mradi huu unawapa wabunifu hawa jukwaa la kuonesha mawazo yao, kuwapatia soko la bunifu zao na hivyo kuwafikia walengwa kwa wepesi. Kwa kuwa maendeleo ya dunia yetu hutegemea kwa kiasi kikubwa uwepo wa wabunifu,wavumbuzi na wagunduzi basi wabunifu hawa wanaosaidia kukuza sekta ya kilimo hutambuliwa, kutangazwa na kujengewa uwezo wa kukuza ubunifu wao. 


Mradi wa Wajasiriamali Wabunifu ni nini?

Mradi huu ni mpango ambao unaruhusu wajasiriamali, wakulima na wavumbuzi wa mbinu bora, rahisi na nafuu za  kilimo kujisajili, kutambulika na  kuonesha ubunifu wao. Iwe unakuza teknolojia bora za kilimo, mbinu za kipekee za kilimo-hai, au bidhaa za kilimo zilizoongezwa thamani, mradi huu ni jukwaa la kuibua wabunifu, kuwalea na kuwatangaza ili wanufaike na ubunifu wao kwa kubadili ubunifu wao kuwa biashara ambayo inaweza kukuza ustawi katika jamii huku ikileta mapinduzi makubwa katika sekta ya kilimo na ufugaji.


Jinsi Mchakato wa Usajili Wa Wabunifu  Unavyofanya kazi

 

Hatua ya 1: Tuma Ombi La Kujisajili Kama Mjasiriamali Mbunifu

Wajasiriamali na wakulima wanaovutiwa wanaweza kujiandikisha kwa kutuma maombi mtandaoni kupitia tovuti ya:  www.ajefarms.com , kupiga simu kupitia +255 743-812-853 au kwa kutembelea ofisi zetu halisi au kupitia mawakala wetu walio katika mikoa na nchi mbalimbali. Waombaji wanatakiwa kuwasilisha:-

  • Jina Kamili & Maelezo ya Mawasiliano
  • Jina la Biashara au Shamba
  • Maelezo ya Ubunifu au Wazo la Biashara
  • Mahali na Sekta ya Uendeshaji
  • Picha au Video Zinazoonyesha Ubunifu husika

Hatua ya 2: Malipo ya Ada ya Uanachama

Ili kuhakikisha mbunifu anafikiwa ni mbunifu huyu hulipa gharama kidogo kwa akaunti maalum za AJE-FARMS mara baada ya hatua ya 1 na ya 2. 

Hatua ya 3: Kusajiliwa, Kutambuliwa Rasmi Na Kutangazwa

Hii hufanyika mara baada ya timu yetu ya wataalamu kufuatilia kwa kina juu ya taarifa za mbunifu na kumfanyia usahili (interview) kabla ya kumpatia kitambulisho maalum cha ubunifu. Mara baada ya kupewa kitambulisho mbunifu huyu huanza kujengewa uwezo zaidi na kutangazwa ili aanze kutoa mafunzo kwa wakulima/wafugaji/wajasiriamali wengine. Pia huunganishwa na fursa nyingine za kukuza ubunifu wake kupitia mikopo au wawekezaji wa kuendeleza ubunifu huo ili kuwa biashara kubwa.

 


Fursa kwa Wakulima na Wajasiriamali Waliosajiliwa

 

1. Kuonesha Ubunifu           

Wanachama waliojiandikisha wanaweza kuonyesha suluhu zao za ubunifu kwenye mfumo wetu wa kidijitali na katika matukio ya maonesho, ikijumuisha:

  • Teknolojia ya Kilimo au Ufugaji Smart – Kuongeza kipato kwa kutoa mafunzo kwa wengine (kwa mfano, mbinu za ubunifu za ufugaji pamoja na zana za kilimo cha usahihi, mifumo ya umwagiliaji ya kiotomatiki n.k)
  • Mbinu za Kipekee za Kilimo Hai na Endelevu
  • Bidhaa za Ongezeko la Thamani (km, mbolea za kikaboni, usindikaji wa chakula, suluhu za shamba au ufugaji)
  • Dhana za Utalii wa Kilimo na Miundo Endelevu ya Biashara ya Kilimo

2. Mitandao na Ushirikiano

Wanachama wanapata ufikiaji wa mtandao wa AJE-FARMS wa wajasiriamali, wawekezaji, na wataalam wa biashara ya kilimo, na hivyo kukuza  ushirikiano wa kibiashara. Wanaweza:

  • Kujiunga na vikundi vya uvumbuzi wa kilimo
  • Kuongeza kipato kwa kushiriki katika programu za ushauri
  • Kushiriki katika vipindi vya kubadilishana maarifa

3. Masoko na Kufahamika/Exposure

Mradi wa MJASIRIAMALI MBUNIFU hutoa majukwaa ya kusaidia wavumbuzi kufikia hadhira pana kupitia:

  • Tovuti yetu na njia za mitandao ya kijamii
  • Masoko na maonesho ya wakulima
  • Maonesho ya biashara ya kimataifa

4. Msaada wa Mafunzo na Maendeleo ya Biashara

Wajasiriamali hupokea mafunzo yanayoendelea, warsha, na huduma za ushauri wa biashara katika maeneo kama vile:

  • Chapa na Ufungaji wa Bidhaa
  • Upatikanaji wa Fedha na Utayari wa Uwekezaji
  • Mikakati ya Upanuzi wa Soko la Bunifu

Kwa nini Ujiunge na Mpango wa Wajasiriamali Wabunifu na Wakulima wa AJE-FARMS?

  • Ada nafuu za uanachama wenye faida za thamani ya juu
  • Upatikanaji wa fursa za fedha na uwekezaji
  • Fursa za kuongeza ubia wa biashara ya kilimo
  • Ushauri kutoka kwa wataalam wa tasnia za ujasiriamali
  • Kutambuliwa kama mvumbuzi/mbunifu wa kilimo/ufugaji

"Hadithi za Mafanikio"

Joseph – Kahama, Shinyanga., kutotoresha mayai Kutumia Pumba

Joseph alitengeneza njia bunifu ya kutotoresha mayai kwa kutumia pumba ambayo imesaidia wafugaji wengi kuzalisha kuku bila ya kutegemea mashine za kutotoresha mayai (incubators). Kupitia programu ya MB, ameweza kufundisha wafugaji wengine kwa ada ndogo, na imesaidia kupata wanaotaka kujifunza ubunifu wake, na kukuza biashara yake kote Tanzania na nchi jirani.

Soma Zaidi Kuhusu Ubunifu Wake Kwa Kubonyeza Hapa

 

 

Mama Kuku - DODOMA., Mjasiriamali Mbunifu wa Kuku Vijogoo 

Mama huyu maarufu kama mama Kuku Vijogoo ameweza kubadili utaratibu wa kuchoma kuku vijogoo ambao uliokuwepo hapo awali kwani watu waliamini kuwa kuku hawa hawawezi kufugwa na kunenepa wakaweza kuvunwa ndani ya kipindi cha miezi 3 tu wakiwa na uzito wa kilo 2 hadi 2.5. Isitoshe kuku hawa hufugwa kwa gharama ndogo zaidi ya aina nyingine ya kuku na huku wakiwa na soko zuri sana mithili ya kuku kienyeji. Mama huyu ni mjasiriamali mbunifu.

Tazama A - Z Kuhusu  Ubunifu Wake Kwa Kubonyeza Hapa:


Jiandikishe Leo!

Je, wewe ni mkulima au mjasiriamali mwenye wazo la kibunifu? Jiunge na Mpango wa Wajasiriamali na Wakulima Wabunifu wa AJE-FARMS leo na ubadilishe ubunifu wako kuwa biashara kubwa !

Bonyeza Hapa kujisajili kama Mjasiriamali mbunifu

 

Jiandikishe Kupata Mafunzo!

Na Je, wewe Mjasiriamali, mkulima au mfugaji na ungependa kujifunza ujuzi wowote kutoka kwa wabunifu.

Bonyeza hapa kujisajili Kupata Mafunzo.

 

Wasiliana Nasi Sasa:
Simu: +255 743 812 853
Barua pepe: info@aje-farms.com
Tovuti:
www.ajefarms.com