
JOSEPH; MFUGAJI WA KUKU ALIYEBUNI MFUMO WA KUTOTORESHA MAYAI KWA KUTUMIA PUMBA
Joseph Daud kijana wa miaka 30 ambaye aliishia darasa la tatu hivi karibuni ameleta gumzo katika jamii ya wafugaji kwa kubuni mfumo wa utotoreshaji mayai kwa kutumia pumba. tu !
Utashangaa kujifunza ubunifu wa kijana huyu licha ya kuwa mlemavu wa mkono wa kulia na mguu wake wa kulia tangu kuzaliwa na kupata maambukizi ya polio.
Bila mashine au incubator kijana huyu aliwezaje kugundua mfumo huu wa kutotoresha mayai kwa kutumia incubator wakati hana elimu yoyote ya mifugo?
Ni kama kuna miujiza ya hawa watu ambao hawamalizi shule "drop outs" kuibuka na ugunduzi mkubwa ! Si kwa Joseph tu ; bali hata Mark Zuckerbag "sonko" wa Facebook hakumaliza shule; Bill Gates hakumaliza shule; Jack Ma wa Alibaba alikuwa mwanafunzi aliyechukuliwa kama kilaza darasani na wengine wengi walichukuliwa poa lakini wakaibukia mtaani na ugunduzi uliotikisa ulimwengu.
Joseph mara baada ya kusimama shule akiwa darasa la tatu aliamua kuishi na wazazi wake kijijini na kuendelea kuwasaidia kwa kazi za shambani; na alipofikisha miaka 20 ndipo akaanza kujitegemea na sasa ni baba wa watoto wanne na mke mmoja akiishi wilayani Kahama pamoja na familia yake. Tangu alipoanza kujitegemea alifanya kazi zile zile za wazazi wake ikiwa ni pamoja na kilimo na ufugaji hasa wa kuku.
Anakiri mwanzoni alikata tamaa kwa sababu ya vifo vingi vya kuku kwa sababu ya magonjwa ambayo alikuwa anashindwa kuyadhiti na huku dawa za madukani zikiwa ni gharama kubwa na zenye masharti magumu ; nyingine zimeandikwa Kingereza wakati yeye lugha hiyo haijui. Baada ya vifo vingi vya kuku alikata tamaa na kuamua kutafuta kazi nchini Kenya katika jiji la Nairobi; nako huko mambo yaligonga mwamba na mwishowe akaona arudi kijijini na kujishughulisha na ujasiriamali wa kupika chipsi. Nako pia mambo yakaenda mrama! Joseph hakukata tamaa na mwishowe akaamua kurudi kijijini rasmi mwaka 2021 kwa ajili ya kilimo cha alizeti, muhogo na ufugaji wa kuku .
Katika ufugaji wa kuku alizoea kuchukua mayai na kuyatunza kwenye pumba ili kuku waweze kutaga vizuri ndipo siku moja alipoamua kuyapima kwa tochi na kugundua kuwa yana kiini chenye kifaranga na akashangaa imekuwaje! Ugunduzi wake ulianzia hapo na mengine yanabakia kuwa ni historia. Tangu hapo aligundua kuwa angeweza kutotoresha mayai ya kuku au ndege wengine kwa kutumia pumba tu! Eureka , Eureka kama alivyosema Mwanasayansi Archimedes aliyegundua kwa nini meli inaelea na shilingi inazama majini! Na akawa kama Isaack Newton aliyegundua kwa nini kitu kikirushwa juu huanguka chini na hakielekei juu.
Anatumiaje Ugunduzi Huu Kwa Manufaa Yake na Jamii Yake?
Tangu Joseph alivyobuni mfumo huu maisha yake yamebadilika pamoja na familia na jamii yake kwa ujumla. Ameweza kuongeza idadi ya kuku kwa kununua mayai kutoka kwa wafugaji wengine na kuweza kupata vifaranga wengi kwa pmaoja na huku akiwafundisha wafugaji wengine juu ya mfumo huu wa asili wa utotoreshaji wa mayai. Na sasa ana amefungua kampuni yake ambayo ameiita "SHOW ME THE MONEY". Na sasa amejisajili rasmi katika mradi wa MJASIRIAMALI MBUNIFU chini ya kampuni ya AJE-FARMS . Na sasa kupitia mradi huu tayari anaendesha mafunzo mtandaoni na kwa kusafiri mikoa mbalimbali nchini Tanzania kwa ajili ya kuwafikia wafugaji wengine. Amezidi kujipaatia umaarufu, kipato na muhimu zaidi kuwakomboa wafugaji wa kuku kuepuka kuku/ndege wengine kuharibu mayai wakati wa kuatamia; kuokoa vipato vyao ambavyo vingetumika kununua mashine za kutotoresha mayai (incubators) na kukabiliana na gharama kubwa za umeme wa kuendesha mashine hizi za kutotoresha mayai.
Vipi Joseph Amewezaje Kudhibiti Vifo Vya Kuku?
Sambamba na kugundua mfumo asili wa kutotoresha mayai kwa njia ya pumba; kijana huyu mbunifu amegundua aina 15 za miti shamba ambazo huzitumia kwa ajili ya kutibu kuku wake. Na sasa hana vifo vya kuku shambani kwake.
Je ungependa kumtembelea shambani kwake Kahama au kujifunza kutoka kwake kupitia mtandao au pengine unahitaji akufikie shambani kwako na mfanye mafunzo kwa vitendo kwa siku 21 pekee tangu yai hadi kupata kifaranga? Tuandikie maoni yako. Au wasiliana nasi kwa simu: +255 743 812853 .
AJE-FARMS; MASHAMBA YANAYOTEMBEA.
5 comments | Jumbe
Mpo kahama sehemu gani?
Niunge
Tumia link hii hapa ili kujaza fomu na kujiunga:
https://docs.google.com/forms/d/e/1FAIpQLScN8Vcu453-XyXl-mRmEyfcVUEd7CO_XiZudds5T7LZkdXGhQ/viewform?usp=header
Karibu sana Mr. Busunda – utachangia ada kidogo.
Kuna njia tatu za kupata mafunzo ikiwa
(01.) unahitaji mkufunzi afike shambani kwako kukufundisha unalipia nauli ya kwenda na kurudi, malazi na chakula na ada ya mafunzo ni TZS 100,000 kwa mafunzo ya siku 21 na
(02.) Ikiwa utakuja kujifunza wewe mwenyewe Kahama unalipia ada ya mafunzo TZS 100,000 kwa siku 21
(3.) Ikiwa unahitaji mafunzo haya uyapate kwa njia ya Mtandaoni yaani WhatsApp/kwa simu ada yake ni TZS 95,000 kwa siku 21.
Napenda kujifunza nami ujuzi huu