DASE FARMS

 


1. Wasifu Mfupi Wa "Shamba Darasa"

  • Jina la mwanzilishi: DASE JAJA SHIMBI
  • Mahali: NYAKAKARANGO, KATOMA B, CHATO, GEITA - TANZANIA
  • Uzoefu: Miaka 30
  • Aina ya Kilimo/Ufugaji: 

Kilimo: Mpunga na Mahindi.

Ufugaji: Kuku Kuchi mwamba, Ng'ombe, Mbuzi, Kondoo.

2. Muhtasari wa Shamba darasa

  • Jina la Mradi/Biashara

DASE FARMS

  • Chanzo

Mwaka 1993 nilianza kufuga kuku pilipili, aina ya pilipili wateja wake wakubwa ilikuwa ni wapemba kwa ajili ya michezo ya kugombanisha. Baadae Nikaamua kufuga kuku kuchi "mwamba" kibiashara. Tangu hapo nimekuwa nikifuga kuchi mwamba mpaka leo hii.

  • Ukubwa wa Ufugaji/Shamba lako:

Nina shamba (Mbuga) inayopatikana Genge kijijini Chato ambayo ni ekari 20, shamba la mpunga lililopo Nyamirembe ekari 25, nafanya kilimo cha mahindi hapa Nyamirembe ambalo ni ekari 15.

Ninafuga Kuku Kuchi aina ya Mwamba ambao wapo zaidi ya 200, Ng'ombe 70, mbuzi na Kondoo kwa ujumla ni 150.

  • Mazao yaliyopandwa na Mifugo inayofugwa katika shamba hili:
KILIMO CHA CHAKULA: chikichi, embe, fenesi, ndimu, machungwa, stafeli, topetope, korosho, minazi, nanasi, pasheni, viazi vikuu, mihogo, tikiti maji n.k. , ufugaji wa mifugo kama vile kuku, bata, samaki, kanga, njiwa nk. ufugaji wa nyuki na uzalishaji wa asali nta na sumu ya nyuki, mazao ya misitu kama mikaratusi, mikangazi, misonobari, mitiki, na michongoma. 
  • Mbinu za Kilimo na ufugaji:

Mbinu za kilimo: nalima mazao na kuweka store - mahindi navuna mwezi wa 5 na kuuza mwezi wa 10. nalima mwezi wa 10-11, kuvuna mwezi 5-6, na kuuza mwezi wa 2-3.

3. Maono na Malengo ya Mkulima

 

       Malengo:

       1. MALENGO YA MUDA MREFU

Bwawa katika shamba la mpunga la nyamirembe, pia kutengeneza nyumba za wageni kutokana na pesa nayopata kwenye kuuza .kuku kuchi na maza

      2. MALENGO YA MUDA MFUPI

kuhifadhi mazao na kuyauza wakati wa soko linapokuwa zuri.



4. Manufaa kwa Jamii Inayozunguka Mradi 

i. Ushirikiano wa Jamii:

(Nyakakarango)msaada wa chakula katika shule ya msingi Nyakakarango. Nimetoa ajira ya watu 34. Kuanzia mwaka 2000 mpaka 2025 nimeweza kuwapatia ajira/vibarua karibia watu 375 katika jamii inayonizunguka.

ii. Wakulima waliofunzwa:

Zaidi ya watu 20 wamefaidika na mbinu nazotumia katika ufugaji wa kuku kuchi pamoja na kilimo cha mpunga na mahindi .

iii. Kazi Nyinginezo Katika Shamba Hili

 

 

5. Mafanikio Ya DASE FARMS:

 

6. Jinsi DASE  FARMS Inavyochangamkia Fursa Za Utalii wa Kilimo, Mila, Utamaduni na Asili

  • Vivutio vya Utalii Vilivyopo LUJUMO FARMS
  1. Vyakula vya asili vya ZIWA VICTORIA mf. Sato, Sangara, parachichi, ndizi bukoba.
  2. Uwepo wa hifadhi ya taifa ya Burigi (
  3. Njia za kiasili za ufugaji na kilimo
 

 Wito Kwa Jamii (CALL TO ACTION)

  • Tembelea DASE FARMS:

DASE FARMS ipo chini ya usimamizi wa mradi wa SHAMBA DARASA. Jamii inapaswa kutembelea shamba hili kujifunza kwa vitendo juu ya mbinu bora za kilimo biashara kwa mazao kama vile   

Una wazo la kufanya kazi au Kushiriana na DASE FARMS?

DASE FARMS inawakaribisha wanaohitaji kazi mashambani, wanunuzi wa mazao na wawekezaji. 

 

ZAIDI KUHUSU DASE FARMS:

  • Ungependa Kujifunza zaidi juu ya namna DASE FARMS inavyosaidia Jamii na juu ya matukio shambani? Usikose kufuatilia stori mashambani kupitia  www.ajefarms.com au WhatsApp: +255 743 812 853.