LUJUMO FARMS

1. Wasifu Mfupi Wa Shamba

  • Jina la mwanzilishi: MANG’OHA LUNYALULA LUCAS
  • Mahali: Bukombe, Geita - Tanzania
  • Uzoefu: Miaka 10
  • Aina ya Kilimo: Lujumo Farms inajishughulisha na kilimo cha Matunda pilipili, parachichi papai na pensheni. 

2. Muhtasari wa Shamba darasa

  • Ukubwa wa Kiwanja/Shamba lako:

Lujumo farms ina ekari zisizo pungua 50

  • Mazao yaliyopandwa na Mifugo inayofugwa katika shamba hili:
PILIPILI, PARACHICHI, PAPAI NA PENSHENI
  • Mbinu za Kilimo na ufugaji:

Miche yote imezalishwa kwa teknolojia ya kisasa kupata mbegu ambayo ni bora zaidi, himilivu zaidi na yenye matunda mengi na makubwa.

3. Maono na Malengo ya Mkulima

      Maono:

Kuwa mfano wa kuigwa katika uzalishaji wa mazao ya kilimo, ufugaji na utunzaji wa mazingira na uzalishaji na utumiaji wa nishati safi.

       Malengo:

       1. MALENGO YA MUDA MREFU

LUJUMO FARMS ina mikakati ya muda mfupi na mrefu ya kuongeza thamani ya mazao yazalishwayo shambani mfano badala ya kuuza kuku iuzwe nyama ya kuku na badala ya kuuza mahindi uuzwe unga wa mahindi kupitia uchakataji katika kiwanda shambani.

      2. MALENGO YA MUDA MFUPI

Kujenga miundombinu ya kuzalisha na kuhifadhi mazao kwani mazao zaidi ya 40% katika mashamba mengi hupotea baada ya mavuno. Ukitembelea LUJUMO FARMS utajifunza mbinu za kuhifadhi mazao kwa usalama mara baada ya mavuno.



4. Manufaa kwa Jamii Inayozunguka Mradi 

i. Ushirikiano wa Jamii:

Mpaka sasa mradi umekwishatoa ajira kwa vijana 4 pale shambani na ni matarajio  kuwa zaidi ya wananchi 100 watafaidika na mradi huu ndani ya kipindi cha mwaka 1.

ii. Wakulima waliofunzwa:

Zaidi ya wakulima wadogo 50 wamefaidika na wengine bado wanaendelea kufaidika kwa kupata mafunzo na kujifunza jinsi ya kufanya kilimo kuwa biashara rasmi kupitia mafunzo katika shamba hili.

iii. Kazi Nyinginezo Katika Shamba Hili

Utoaji wa elimu ya kilimo hasa pesheni, pilipili, parachichi na papai pamoja na ufugaji. Kukodisha mashamba, kulima, kupanda mazao, kusafirisha mazao ya kilimo, utafiti wa masoko ya mazao ya kilimo na mifugo, kutoa ushauri na elimu ya afya lishe na mitindo ya maisha, uzalishaji wa miche aina zote, ustawishaji wa mazao kama papai, pesheni, parachichi, na pilipili.

5. Mafanikio Ya LUJUMO FARMS:

LLUJUMO FARMS mpaka sasa imeweza kuiendesha miradi yake hii kupitia vyanzo vikuu viwili, ikiwemo kutoka katika akiba binafsi kutoka kwa mkurugenzi wake. Pia Mpaka sasa mradi umekwisha toa ajira kwa vijana 4 pale shambani na ni matarajio yetu kuwa zaidi ya watu 100 watafaidika na mradi huu ndani ya kipindi kifupi.

6. Jinsi LUJUMO FARMS Inavyochangamkia Fursa Za Utalii wa Kilimo, Mila, Utamaduni na Asili

  • Vivutio vya Utalii Vilivyopo LUJUMO FARMS

  1. Vyakula vya asili vya kabila la Wasukuma mfano michembe, udaga n.k
  2. Uwepo wa Mbuga Ya Wanyama Burigi Chato kwani shamba hili limepakana kabisa na Hifadhi hii na hivyo ukitembelea shamba hili utawaona wanyama bila kulipia gharama za Hifadhi; raha iliyoje.
  3. Njia za kiasili za ufugaji na kilimo
  4. Ngoma za asili kama "Chagulaga"
 

 Wito Kwa Jamii (CALL TO ACTION)

  • Tembelea LUJUMO FARMS:

LUJUMO FARMS ipo chini ya usimamizi wa mradi wa SHAMBA DARASA. Jamii inapaswa kutembelea shamba hili kujifunza kwa vitendo juu ya mbinu bora za kilimo biashara kwa mazao kama vile  pesheni, pilipili, parachichi na papai pamoja na ufugaji.

Una wazo la kufanya kazi au Kushiriana na LUJUMO FARMS?

LUJUMO FARMS inawakaribisha wanaohitaji kazi mashambani, wanunuzi wa mazao na wawekezaji. 

 

ZAIDI KUHUSU LUJUMO FARMS:

  • Ungependa Kujifunza zaidi juu ya namna LUJUMO FARMS inavyosaidia Jamii na juu ya matukio shambani? Usikose kufuatilia stori mashambani kupitia  www.ajefarms.com au WhatsApp: +255 743 812 853.