KAF FARMS

 

1. Wasifu Mfupi Wa Shamba

  • Jina la mwanzilishi: Yasini Athuman Kilima
  • Mahali: Bagamoyo, Pwani - Tanzania
  • Uzoefu: Miaka 15
  • Aina ya Kilimo: 

KAF Farms inajishughulisha na kilimo cha mazao ya chakula, mifugo, na misitu.

2. Muhtasari wa Shamba darasa

  • Jina la Mradi/Biashara

KILIMA AGROPIARY FARMS/KAF FARMS

  • Ukubwa wa Kiwanja/Shamba lako:

KAF FRMS ina ekari zisizo pungua 100.

  • Mazao yaliyopandwa na Mifugo inayofugwa katika shamba hili:
KILIMO CHA CHAKULA: chikichi, embe, fenesi, ndimu, machungwa, stafeli, topetope, korosho, minazi, nanasi, pasheni, viazi vikuu, mihogo, tikiti maji n.k. , ufugaji wa mifugo kama vile kuku, bata, samaki, kanga, njiwa nk. ufugaji wa nyuki na uzalishaji wa asali nta na sumu ya nyuki, mazao ya misitu kama mikaratusi, mikangazi, misonobari, mitiki, na michongoma. 
  • Mbinu za Kilimo na ufugaji:

KAF itatumia jukwaa la wataalamu wetu na washirika kwa kutoa huduma mbalimbali zinazohusiana na kilimo, ufugaji mf. SHAMBA DARASA pamoja na kusaka masoko ndani na nje ya mipaka ya Tanzania.

3. Maono na Malengo ya Mkulima

      Maono:

  • Utoaji wa elimu ya jinsi ya kuzalisha na kutumia nishati safi ili kuepuka matumizi ya kuni na mkaa. Kufanya utafiti wa kuzalisha kutumia mbolea ya kijani(Organic Fertilizer) itokanayo na takataka za shambani na mifugo ikiwemo taka zitokanazo na Biogas na kupunguza kabisa matumizi ya mbolea za kemikali.
  • Kujikita katika utafiti wa kuzalisha na kutumia viuatilifu vinavyotokana na mazao yashambani na mabaki yake ili kuepuka matumizi ya viuatilifu vya kemikali za viwandani katika kulinda afya za walaji na kuepuka kudhuru nyuki kwa kutumia sumu katika kupulizia mazao.
  • Kuzalisha mbegu za asili za mazao kama mpunga, mahindi, maharage ili kuepuka kutumia mbegu hatarishi zilizobadilishwa viasili (GMO) ambazo zinaweza kuathiri walaji.

       Malengo:

       1. MALENGO YA MUDA MREFU

Kufanya mradi wa KAF Farms kufikia mikoa mingi zaidi Tanzania bara na visiwani. Kuifanya KAF farms kuwa wenye mfumo bora ambao unaweza kutumika hata katika Franchising.

      2. MALENGO YA MUDA MFUPI

Kurasimisha mashamba yetu yaliyopo Bagamoyo, Kiwangwa na Tabora. Kuongeza kilimo kwenye mazao yenye tija pamoja na kuongeza uzalishaji wa mazao ya nyuki kwa kuongeza mizinga. Kuongeza wataalamu wa nyanja tofauti tofauti katika mradi huu ili kuongeza ufanisi na weledi.



4. Manufaa kwa Jamii Inayozunguka Mradi 

i. Ushirikiano wa Jamii:

KAF FARMS Imeajiri vijana wasiopungua 10 mashambani. Maatarajio yetu ni kuwafikia wananchi wa karibu ya shamba 100 watafaidika na mradi huu ndani ya kipindi cha mwaka 1.

ii. Wakulima waliofunzwa:

Zaidi ya watu 30 wamefaidika na KAF FARMS na tunategemea wakulima wengi zaidi watakuja kujifunza kuhusu kilimo biashara.

iii. Kazi Nyinginezo Katika Shamba Hili

Pia KAF Farms ina mpango wa kuanzisha kilimo cha uyoga na uzalishaji wa mbolea itokanayo na takataka za mfumo wa uzalishaji wa uyoga pamoja na mazao mengine shambani kama vile masalia ya mimea na takataka za mifugo. Pia KAF farms inatarajia kuanzisha mradi wa nishati safi itokanayo na kinyesi cha mifugo na mabaki ya mbogamboga (BioGas) ambayo kwa kuanza itatumika kama nishati katika kuzalisha mafuta ya chikichi na matumizi mengine yanayohitaji nishati hapo shambani.

5. Mafanikio Ya KAF FARMS:

KAF Farms - Makurunge ni shamba lenye ekari 40 za mraba. Mradi huu una miaka 6 Tumefanikiwa kuotesha zao la michikichi ipatayo 300 mizinga ya nyuki 70 miembe 2000, mikorosho ekari 3, mikaratusi, migomba, maembe ekari 3, minazi, mastafeli pamoja na fenesi.

6. Jinsi KAF  FARMS Inavyochangamkia Fursa Za Utalii wa Kilimo, Mila, Utamaduni na Asili

  • Vivutio vya Utalii Vilivyopo LUJUMO FARMS

  1. Vyakula vya asili vya watu wa pwani.
  2. Uwepo wa Apiary Farms/shamba la michikichi
  3. Njia za kiasili za ufugaji na kilimo
  4. Shamba la miti ya misitu
 

 Wito Kwa Jamii (CALL TO ACTION)

  • Tembelea KAF FARMS:

KAF FARMS ipo chini ya usimamizi wa mradi wa SHAMBA DARASA. Jamii inapaswa kutembelea shamba hili kujifunza kwa vitendo juu ya mbinu bora za kilimo biashara kwa mazao kama vile   

Una wazo la kufanya kazi au Kushiriana na KAF FARMS?

KAF FARMS inawakaribisha wanaohitaji kazi mashambani, wanunuzi wa mazao na wawekezaji. 

 

ZAIDI KUHUSU KAF FARMS:

  • Ungependa Kujifunza zaidi juu ya namna KAF FARMS inavyosaidia Jamii na juu ya matukio shambani? Usikose kufuatilia stori mashambani kupitia  www.ajefarms.com au WhatsApp: +255 743 812 853.