SHAMBA DARASA
Muhtasari wa Mradi wa Shamba Darasa
"Kuwawezesha Wakulima Wadogo Kupitia Mafunzo na Ubunifu"
Utangulizi
Mradi wa Shamba Darasa (Demo Farm Project) ni mpango wa mageuzi uliobuniwa kuwapa wakulima wadogo maarifa na kuwawezesha kupata zana za kilimo na rasilimali zinazohitajika ili kuongeza tija katika kilimo pamoja na kufuata kanuni za kilimo endelevu. Kwa kuanzisha Mashamba Darasa katika mikoa muhimu kote Tanzania pamoja na nchi jirani. Mashamba haya katika mradi huu yatatumika kama vitovu vya kujifunzia kwa vitendo ambapo wakulima/wafugaji wanaweza kupata uzoefu wa vitendo na kujifunza mbinu za kisasa za kilimo zinazolingana na mazingira yao kwa kuzingatia usalama wao, walaji wa mazao yao na mazingira kwa ujumla.
Mradi huu unatekelezwa katika mikoa yote ya Tanzania. Mradi wa Mashamba Darasa haya utaonesha mbinu bunifu za kilimo, kuwezesha wakulima kufikia pembejeo, zana za kilimo na teknolojia ; sambamba na kuunganisha wakulima/wafugaji na masoko yenye tija.
Malengo ya Mradi
LENGO KUU:
Kukuza uchumi wa wakulima kwa kuongeza uzalishaji wa mazao bora na utunzaji wa mazingira
kupitia utoaji wa elimu kwa vitendo mashambani.
MALENGO MADOGO YA MRADI WA SHAMBA DARASA:-
i. Kutambua hali ya uchumi ya wakulima na masoko ya mazao.
ii. Kutambua mbinu wanazozitumia wakulima katika uzalishaji.
iii. Kutambua mbinu wakulima wanazotumia kutunza mazingira huku wakijilinda
wenyewe na walaji wa mazao yazalishwayo shambani
iv. Kuanzisha mashamba darasa ya mazao muhimu kulingana na mazingira ya eneo
husika.v. Kuunda jukwaa la usambazaji/uwasilishaji wa taarifa sahihi za kilimo kwa wakulima.
vi. Kuwaunganisha wakulima na kuunda vikundi mbalimbali vikiwemo vikundi vya mtandao wa kibiashara, vikundi vya kutunza mazingira n.k
vii. Kuanzisha mtandao wa kibiashara baina ya wakulima na wadau mbalimbali ambapo
kupitia mtandao huo wakulima na wafanyabiashara watapata taarifa sahihi na kwa
wakati juu ya upatikanaji wa mazao, pembejeo, elimu, masoko, zana na teknolojia
bora za kilimo na ufugaji. Na hii itawasaidia kufanya maamuzi sahihi.
viii. Kuanzisha programu atamizi (incubation program) kupitia mashamba darasa ambapo vijana na wanawake wataweza kupata elimu kwa vitendo shambani kwa kipindi
maalum kabla ya kwenda kuanzisha miradi yao wenyewe.
Program Mahsusi Katika Mradi Wa Shamba Darasa:
- Program ya Mafunzo kwa Vitendo Mashambani:Kupitia program hii wafanyakazi wa shamba darasa husika watafundishwa na AJE-FARMS ili kuweza kufundisha wakulima wanaofika katika shamba darasa hili kwa ajili ya mafunzo kwa vitendo.
- Program ya Utunzaji wa Mazingira:Wakulima na wafugaji walio katika eneo la kata lilipo shamba darasa wataunda vikundi vya utunzaji wa mazingira kwa kupanda miti, kusafisha maeneo yao n.k.
- Program ya Vituo vya Maonesho:Kupitia program hii bidhaa pamoja na bunifu mbalimbali zitaoneshwa kwenye kituo cha maonesho ya kilimo/ufugaji ambacho kitaanzishwa kila kanda.Vituo hivi vitaonesha vifaa/zana za kilimo, mazao yaliyovunwa, mbegu, miche na teknolojia mbalimbali za kilimo na ufugaji ili kuzisamabaza kwa walengwa kupitia maonesho haya.Vituo hivi pia vitaonesha tamaduni, mila na mbinu za asili za kilimo/ufugaji wa jamii inayozunguka katika eneo hilo. Bidhaa zitakazooneshwa katika kituo hiki ni kutoka kwa wajasiriamali wabunifu na mashamba darasa.
Sifa Muhimu za Mashamba Darasa
Shamba hili sharti liwe lenye umiliki wa kudumu na lisiwe la kukodi; laweza ukubwa wowote kuanzia robo ekari .Liwe linafikika kwa wepesi kipindi chote cha mwaka. Lisiwe na migogoro wala mashitaka yoyote mahakamani.
Faida kwa Wafugaji Na Wakulima Wadogo Na Wa Kati Katika Mradi Wa Shamba Darasa
-
Kuongezeka kwa Tija: Wakulima watajifunza mbinu zinazoboresha mavuno ya mazao na kupunguza gharama.
-
Ufikiaji wa Soko: Ushiriki katika mradi unawaunganisha wakulima na masoko ya uhakika na wanunuzi.
-
Usaidizi wa Kifedha: Kupitia ushirikiano wa Mradi wa Shamba Darasa na Utalii wa Kilimo na Utamaduni, wakulima wananufaika kwa kuunganishwa na taasisi za mikopo ili kusaidia kukuza miradi mashambani. Mradi huu ni daraja la kuunganisha wadau wote muhimu wa kilimo biasharara.
- Shamba Darasa litatangazwa kupitia AJE-FARMS na hivyo kuvutia wawekezaji na wanunuzi wa mazao yazalishwayo shambani hapo.
Ifuatayo ni orodha ya mashamba darasa yaliyosajiliwa hadi sasa.
|
Hitimisho
Mradi wa Shamba Darasa unatoa mtazamo kamili wa kubadilisha kilimo nchini Tanzania na nchi nyingine barani Afrika. Kwa kuchanganya mafunzo ya vitendo, upatikanaji wa rasilimali, na kuongeza ubunifu wa Utalii wa Kilimo na Utamaduni, mpango huu unawawezesha wakulima wadogo kujenga maisha endelevu huku wakichangia maendeleo ya kiuchumi na kiutamaduni katika jamii zao. Kwa pamoja, tunaweza kutengeneza mustakabali mwema kwa kilimo barani Afrika na jamii zetu zote kwa ujumla. Kila mmiliki wa shamba darasa atalazimika kusajili shamba lake ili kuweza kutambuliwa na mradi huu. Kila mmiliki wa shamba darasa mara baada ya kujisajili katika mradi huu atajulikana kama AJE-FARMER na atapewa kitambulisho chenye Namba Maalum ya Kumbukumbu (ID Number); kisha taarifa za shamba/mradi wake zitawekwa katika tovuti ya www.ajefarms.com na kuanza mara moja kushiriki katika mafunzo ya kilimo biashara ikiwa ni pamoja na kupewa ushauri kadri inavyohitajika.
KUJISAJILI
Bonyeza Hapa Kusajili Shamba Lako kuwa Shamba Darasa
Gharama ya kusajili shamba darasa ni TZS 15,000; ilipwe kwa Akaunti ya M-PESA LIPA NAMBA:- 562448 (Jina: AJE-FARMS) Au CRDB A/C # 0150481009500 AJE FARMS CO LTD : SWIFT CODE: CORUTZTZ
Bonyeza Hapa Kujisajili kwa ajili ya ziara ya mafunzo shambani
Gharama ya kufanya ziara ya mafunzo shambani ni TZS 25,000 kwa watanzania na $ 20 kwa kila mshiriki wa mafunzo kwa masaa 8; ilipwe kwa Akaunti ya M-PESA LIPA NAMBA:- 5762448 (Jina: AJE-FARMS)
Au CRDB A/C # 0150481009500
AJE FARMS CO LTD : SWIFT CODE: CORUTZTZ
Ukishajaza tutumie meseji kupitia WhatsApp namba +255 743 812 853