Kupima Udongo Wa Shamba Lako Sasa Imekuwa Ni Rahisi
"Utangulizi"
AJE-FARMS CO.,LTD kwa kushirikiana na kampuni ya LIVE SUPPORT SYSTEMS (T) LTD (LSSL) Tunakukaribisha wewe mkulima ili upime afya ya udongo wa shamba lako ili ujue virutubishe muhimu mfano N.P.K vinavyohitajika kwenye mimea yako ili kukuongezea tija katika mavuno yako.
LENGO / MADHUMUNI
Lengo nikuwasaidia wakulima wote nchini Tanzania kujua afya ya udongo hasa tindikali - (PH) na pia kujua virutubisho vilivyoko katika udongo kabla ya kulima zao lolote ili kufahamu kiasi cha uhitaji wa mbolea inayohitajika katika mimea na pia kujua virutubisho vilivyoko katika udongo kama ni- organic, carbon, nitrogen, sodium, potassium, pamoja na virutubisho vidogo vidogo vilivyoko kwenye udongo ambavyo ni muhimu sana kwa ukuaji na uzalishaji kwa mimea( micro element) - boron, zinc, coper, cobalt, silicon n.k
NAMNA YA KUCHUKUA SAMPULI ZA UDONGO SHAMBANI
- Ni muhimu sana kabla ya kulima na kuotesha mkulima natakiwa kujua afya ya udongo wa shamba lake.
- Unahitaji kuchukua udongo(Sampuli) kwenye shamba lako unalotaka kulima, au kulingana na zao unalotarajia kulima, hii ni kwa sababu kila zao linauhitaji wa mbolea zinazo tofautiana.
- Chukua sampuli za udongo(ZigZag). Chukua sampuli kama utakavyoelekezwa na mtaalamu wetu wakati wa maelekezo.
FAIDA ZA KUPIMA UDONGO
- Kupima udongo kunasaidia kuamua aina ya zao linalofaa kulimwa kwenye shamba lako
- Utajua virutubisho ambavyo viko kwenye udongo na kwa kiasi gani.
- Utanunua mbolea kulingana na upungufu wa virutubisho vinavyohitajika kwenye udongo, wakulima wengi wamekuwa wanatumia mbolea hata kwa mashamba ambayo virutubisho vipo vya kutosha.
- Kutasaidia kutunza mazingira kwa sababu badhi ya virutubisho vikizidi kwenye udongo uweza kuharibu udongo (Residue Effects)
- Kupima udongo kutakusaidia kujua mahitaji kamili ya mbolea / virutubisho.
- Kupima udongo kutakusaidia kujua jinsi ya kuuboresha udongo.
FANYA UAMUZI SAHIHI WA KUPIMA UDONGO WA SHAMBA LAKO; TUPIGIE LEO KUPITIA;
SIMU: +255 743 812 853
WHATSAPP: +255 743 812 853
BARUA PEPE: info@aje-farms.com