Mfugaji wa kuku wa kienyeji mwenye ndoto ya kuwa bilionea

Mfugaji wa kuku wa kienyeji mwenye ndoto ya kuwa bilionea

 

Ujio wa mtandao(internet) umebadili maisha ya kila mmoja wetu. Bi Rahel; mfugaji wa kuku wa kienyeji mkoani Mwanza alipata kuona fursa ya masoko ya kuku wa kienyeji katika mtandao wa AJE-FARMS na kuamua kufanya mawasiliano ambapo aliweza kunufaika na masoko pamoja na kukuza mtandao wake wa kilimo biashara kupitia simu yake kiganjani bila hata kufika ofisini. Kwa furaha na bashasha mara baada ya kufanikiwa kuuza kuku wake wote kwa bei nzuri Bi Rahel alituma ushuhuda wake ofisini kwa njia ya ujumbe wa WhatsApp nasi tunauchapisha hapa kama ifuatavyo- kwa nukuu:-

"Kwa jina naitwa Rahel Petro Emmanuel ninaishi katika Kijiji Cha Ngh'aya kilichopo kata ya Ngh'aya wilaya ya  Magu mkoani mwanza

Kitaaluma Mimi ni Mwalimu,nikiwa Mwalimu pia huwa ninajishugulisha na kilimo Cha Mpunga na ufugaji wa kuku wa kienyeji kwa takribani miaka mitano iliyopita

Nilianza na kuku wachache tu jogoo na tetea wawili baada ya muda wa miezi miwili waliongezeka idadi ndipo nilipo pata wazo la kuanzisha mradi wa ufugaji wa kuku wa kienyeji ili nifuge kama biashara yangu ya nyumbani ili niweze kujipatia kipato katika  familia yangu


Kwanza ilinibidi nionane na mtaalamu wa mifugo hapa kijijini kwetu nikaomba ushauri wa namna nzuri ya kufuga kuku wa kienyeji alinipa mwongozo kwa kuzingatia mambo yafuatayo:-

1:Kuwapa kuku lishe bora ili waweze kutaga mayai mengi hadi mayai ishirini kwa kuku mmoja
2:Kutambua yai lillilo bora ili kupata vifaranga vilivyo Bora

3: Jinsi ya kulea vifaranga kwa kuwatoa kwa mama yao baada ya kutotolewa kwa kutumia jiko la mkaa
4: Kutunza vifaranga kwa kuwapa lishe bora ili wasipatwe na magonjwa
5: kuzingatia chanjo ya vifaranga na kuku wote kwa usahihi kuanzia siku ya kwanza (1_28) na kuendelea
6: Kuzingatia usafi wa banda wanapo lala kuku


Katika hatua hii ya ufugaji wa kuku wa kienyeji kuna changamoto ambazo hujitokeza mfano
1:Upatikanaji  wa chanjo kwa wakati; kuna wakati mwingine unahitaji kuchanja lakini  chanjo husika inakosekana 
katika mazingira yetu inasababisha vifaranga na kuku wengine kufa

2:Gharama za kununua lishe ya vifaranga au chakula cha vifaranga waliotolewa kwa mama yao baada ya kutotolewa

3: Upatikanaji wa soko la kudumu la kuuzia kuku wa kienyeji kwa wakati
 
Kutokana na changamoto hizi ndipo nilipoamua kuwatembelea  majirani zangu na kuwashirikisha kuhusu njia gani tutumie ili tuweze kupata namna nzuri ya kupata chanjo kwa wakati.

Tulikubaliana kuchangia gharama kwa kila chanjo husika na mmoja wetu anaenda kununua inakopatikana pia tukashauriana kushirikishana katika upatikanaji wa soko pale linapopatikana .


Siku moja katika kutafuta soko la kuuzia kuku wa kienyeji mtandaoni niliona chaneli ya  AJE FARMS MASHAMBA YANAYOTEMBEA katika mtandao wa YouTube; nikawauliza kuhusu  soko la kuku wa kienyeji na wakanipa mwongozo wa kuuza kuku wa kienyeji kwa njia ya mtandaoni.
Kiukweli haikuwa rahisi kuamini kuwa  ni sehemu sahihi  ilibidi nimshirikishe na mwenzangu (mume wangu) naye pia hakuamini.

Lakini AJE FARMS walinipigia simu na kunitoa wasiwasi wakaniambia kuwa hii ni kampuni sio mtu binafsi tunafanya biashara ya masoko mtandaoni ya kuuza na kununua bidhaa mbali mbali za kilimo na ufugaji pamoja kuwaunganisha moja kwa moja wauzaji na wanunuzi wa mazao ya kilimo/ufugaji.

Muda  nikiwa sijaamini walinipa tenda ya kusafirisha vifaranga vya kuku wa kienyeji lakini kwa vile nilikuwa sijaamini tenda hiyo ilinipita.

Ilinibidi kuchukua hatua ya kuthubutu""niliwarudia na kuwaambia nipo tayari kufanya nao biashara.
Kwa kweli AJE  FARMS walinipa  moyo sana juu ya soko la kuku wa kienyeji.AJE  FARMS walinisaidia kuuza kuku wangu kwa muda mfupi tu wakaisha hadi ilinibidi kuwaunganisha na wafugaji  wengine katika jamii yangu inayonizunguka kujiunga na AJE  FARMS ili kupata soko kwa uhakika.

Kupitia AJE FARMS MASHAMBA YANAYOTEMBEA nimepata mafanikio ambao hata sikutarajia kuyapata; kwa mfano nimenunua mashine ya kutotoreshea vifaranga yenye uwezo wa kutotoleshea vifaranga 112 kwa wakati mmoja. Hii itanisaidia kukuza kipato cha familia yangu na hata kwa wanajamii wenzangu kwani wataweza kutotoresha vifaranga vyao kisasa na upotevu wa mayai uliokuwa unajitokeza kwa kuatamia kuku mwenyewe itakuwa imeisha

Matarajio yangu katika hatua hii ya ufugaji natamani sana kuwa mfugaji mkubwa wa kuku wa kienyeji na hata ikiwezekana niwe mfugaji wa kimataifa wa kuku wa kienyeji ili niweze kutoa ajira kwa vijana ambao wapo mtaani na hawana ajira ili waweze kujipatia kipato kupitia mradi wa kuku wa kienyeji

Wito wangu kwa wanajamii yote na wafugaji wadogo wadogo wa kuku wa kienyeji tuwe na uthubutu wengi wetu tunaogopa kuwa ufugaji una gharama lakini niwatoe wasiwasi Sasa hivi soko liko wazi kupitia AJE FARMS MASHAMBA YANAYOTEMBEA kikubwa tuzingatie ufugaji wa kisasa ili mifugo yetu iweze kuwa na kiwango kizuri kinacho hitajika katika soko.

Wito kwa serikali na kwa wadau binafsi itushike mkono hasa sisi wanawake kwa kutupatia mitaji ili tuweze kuwekeza katika miradi mikubwa ya kuku wa kienyeji pia kufuga kisasa ilil tujikwamue kiuchumi
Pia hii itasaidia wanawake kutokuwa  tegemezi katika familia kwani ni mradi rahisi ambao mwanamke ataweza kuhudumia familia kikamilifu na muda huohuo ataweza kuhudumia au kusimamia mradi wake wa ufugaji wa kuku wa kienyeji"

Je ungependa kumtembelea Bi Rahel shambani kwake ili kupata kujifunza zaidi juu ya ufugaji wa kuku wa kienyeji bila vifo vya kuku kabisa?

Je una maoni au maswali ? Tafadhali usikose kuandika maoni yako hapa au kututumia ujumbe kwa WhtsApp:- +255 743 812 853

 

Back to blog | Rudi kwenye blogu

Leave a comment | Acha ujumbe